NA FRANCIS.A.MAIGE. 0672-249431
Kufanya maamuzi siku zote ni
jambo gumu sana linalomuweka mtu kwenye wakati mgumu sana,mimi nampenda sana
baba yangu nipo tayari ata kufa kwa ajili yake kwa kuwa nafahamu thamani yake
kwangu,lakini nitaonekanaje kwa wananchi hasa pale ninapo takiwa kufanya mauaji
ya Raisi hili nimuokoe baba yangu asiuawe, japo ni jambo gumu ila mimi nitaweza
tu????.
Usiku majira ya2 :45,katika
nyumba ya moris mlango ukawa unagongwa kwa kishindo kikubwa(ngoo,ngoooo,ngoooo)”hodi,hodi
tusaidieni tunakufa huku”moris akashituka kutoka usingizi na kumuamsha mke kwa
kumtikitisa kwenye mabega na kumuhita,mke wake akaamka kutoka usingizini akiwa
na uchovu huku akiwa anatazamana macho kwa macho na mume wake na kumuuliza.
“kuna nini
mbona umenishitua usiku wote huu” happy akamuuliza mume wake?????
“hapana mke
wangu kuna watu wanagonga mlango ,umesikia hizo kelele za hodi ngoja
nikawasikilize wana tatizo gani usiku huu”.Happy akamzuia mume wake kwa kuofia
wanaweza kuwa ni watu wabaya wasije wakamjeruhi
“hapana mume
wangu usiende wanaweza kukujeruhi”
“hapana
hawawezi kunijeruhi usiogope mpenzi”
“sawa basi
twende pamoja”
“okay twende”
Baada
ya kukubaliana kuwa waende wote pamoja, Happy akavaa vazi la usiku na kujifunga
na kanga kwa kuwa nguo ilikua nyepesi sana yenye kuonyesha umbo lake,kisha wote
wawili wakashuka kutoka kitandani na kuelekea sebureni huku wakiwa na hofu
kubwa misili ya swala aliye bananishwa na chui.Baada ya kufika sebureni moris
akafungua dirisha na kuchungulia nje akawaona vijana wawili wakiwa wamesimama
mlango kwake mke wakiwa wanalia,muda huo huo moris kajawa na uluma ndani ya
moyo wake akaona bora awafungulie hili ajue wanatatizo gani,happy akamsihii mume
wake awe makini wakati anafungua mlango maana bado hawaja wafahamu vizuri hao
wanahitaji msaada,moris akafungua mlango kwa hofu kubwa na kukutana na vijana
wawili wakike na wakiume,akawaribisha ndani na kuketi kwenye sofa huku wakiwa
wanahofu kubwa.morisi na mke wake wakaanza kuzungumza na hao vijana walio
wasaidia,
“poleni sana kwa matatizo”moris
akawauliza huku akiwatizama kwa makini
“asnteni kwa msaada wenu”
“msijal kitu gani kimewakuta usiku huu
na mnatokea wapi…..??????”moris akauliiza
“tumenusulika kuuawa na majambazi pia
sisi ni wakazi wa mbezii beach”
“poleni sana kwa nini mnatakiwa kuuawa “
Vijana hao
wawili wakahuzunika sana na kutiririkwa na machozi ya hasira ikabidi wahadithie
mkasa ulio wakuta mpaka kwa nini wanahitajika kuuawa “katika familia yetu tuko
wawili tu mimi na mdogo wangu Davison(22)Baba na mama yetu walitupenda
sana,siku ya jumatano usiku wakati tumeketi sebureni na mama tukiwa na furaha
kupita kifani mara simu ya kiganjani ya mama ikawa inahita,mama akanyanyuka na
kusogeaa pembeni kidogo na kupokea simu
“hellooo….”
No comments:
Post a Comment