SILAHA
ANANG’ATA KAMA SUARES
MCHEZAJI wa timu ya soka ya Home Boys, Silaha
ibrahimu, juzi alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu baada ya kumng’ata mwenzake
wa Matairi FC.
Silaha alifanya hivyo wakati wa mchezo wa Vijana Cup
uliochezwa kwenye Uwanja wa Kimara, jijini Dar es Salaam ambao ulimalizika kwa
Matairi kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.
Wakati Abdusalam Jamali wa Matairi akielekea kufunga
bao la pili, Silaha alimkaba na kumng’ata kwenye shingo na kufanya mchezaji
huyo kushindwa kuzifumania nyavu.
Mwamuzi Juma Bundala alimfuata mchezaji huyo na
kumpa kadi nyekundu ambapo awali alikuwa ameshapewa kadi ya njano kwa kucheza
rafu uwanjani.
Eti
wamebadilishana jezi dakika ya 65!
WACHEZAJI wa timu ya Nyuki na
Mzinga waliamua kubadilishana jezi wakati mechi ya ligi ya Bodaboda ikiendela
katika Uwanja wa Bwawani Mbezi, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 65
ya mchezo ambapo wachezaji watatu kutoka timu zote walibadilishana jezi na
kuwaacha mashabiki wakiwa midomo wazi.
Walipoulizwa kwanini wamefanya hivyo,
walisema walitaka kufanya tukio mbalo litakuwa la kihistoria katika ligi hiyo
ambayo inaelekea nusu fainali.
Wapinzani
V Wananchi ngoma droo
TIMU za Wapinzani na Wananchi zimeshindwa
kutambiana baada ya kutokufungana katika mchezo wao wa kombe la mbuzi
uliochezwa kwenye Uwanja wa Stop Over, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa
Wapinzani, Daudi Sauti, alisema japo hawakufanikiwa kuona lango la Wananchi,
lakini wachezaji wake wamecheza mpira wa kiwango cha juu na watajipanga vyema
kwenye mchezo ujao.
Wacomoro
wa Yanga wasepa na boda boda ya mtu
KIJANA Saidi Mkakazi mkazi wa
Ubungo RiverSide, alijikuta akiangua kilio kwa kile kilichotokea baada ya Ngaya
kuchapwa mabao 5-1 na Yanga.
Kabla ya mchezo huo uliochezwa
Comoro, kijana huyo alibisha na kusema kuwa mara nyingi Yanga huwa inafungwa inapotoka
nje ya Tanzania.
Said alikwenda mbali zaidi na kutoa
Bodaboda yake akisema kama Yanga watashinda basi ichukuliwe na aliokuwa
akibishana nao.
Bada ya Ngaya kukubali kichapo
ikiwa ugenini, madereva wenzake walichukua boda boda hiyo, kitendo
kilichomfanya kuangua kilio kama mtu aliyefiwa.
Hata hivyo, wenzake walimwonea
huruma na kumrudishia mali yake hiyo na ndipo walipomuonya kubeti.
No comments:
Post a Comment